Barua Pepe | Facebook | Instagram | Twitter |

Elimu ya Afya kwa Umma

ELIMU YA LISHE

Lishe bora maana yake ni kula chakula cha kutosha na chakula chenye virutubisho vyote muhimu. Lishe bora  husaidia mwili kukua vyema, kuujenga mwili lakini pia huimarisha kinga ya mwili ili kuweza  kupigana na magonjwa. Ili lishe iwe bora ni muhimu iwe na mchanganyiko wa vyakula mbalimbali kama vile protini, wanga, fati, mbogamboga, madini, matunda na maji kwa wingi .

read more
ELIMU YA MAGONJWA YA TUMBO YANAYOSABABISHA KUHARISHA

Magonjwa haya ni kama vile homa ya tumbo (typhoid), kipindupindu, amoeba na minyoo. Haya ni magonjwa yanayosumbua jamii zetu kwa kiwango kikubwa. Yanasababishwa na kunywa au kula chakula chenye vimelea vya magonjwa hayo.

NJIA YA KUSAMBAA KWA MAGONJWA HAYA NI KAMA VILE;

1.Kula chakula au kunywa kinywaji kilicho na vimelea vya ugonjwa

Kunywa maji ambayo hayajachemshwa

Kula chakula kilichoandaliwa mazingira ambayo siyo safi

Kula matunda na mboga mboga ambazo hazijaoshwa vizuri

Kula chakula ambacho hakijafunikwa na kimepoa

2.Kutofuata kanuni na miongozo ya unawaji wa mikono

Kunawa mikono kwenye chombo kimoja

Kulisha mtoto bila kunawa mikono kwa sabuni na maji tiririka

Kutonawa mikono baada ya kutoka chooni

Kula chakula bila kunawa mikono kwa maji na sabuni

Kuandaa chakula bila kusafisha mikono

Mama kutonawa mikono baada ya kushika kinyesi cha mtoto

3.Kutofuata ujenzi  wa choo bora na matumizi sahihi ya choo

4.Kuchafua vyanzo vya maji kwa kutirirsha maji ya choo kuelekeza kwenye mito na mifereji

5.Utupaji hovyo wa taka katika mazingira yetu kama vile majumbani,sokoni na minadani

NJIA YA KUJIKINGA NA MAGONJWA HAYA NI KAMA VILE;

1.Kusafisha mazingira yetu na kutoa taka zote ambazo ni hatari kwa afya zetu

2.Kuchemsha maji ya kunywa na kuhifadhi katika chombo kisafi chenye mfuniko imara

3.Kuandaa chakula katika mazingira safi na kukifunika kabla hakijatumika

4.Safisha vizuri kwa maji safi na tiririrka vyakula vinavoliwa vibichi kama vile matunda, mbogamboga na saladi (kachumbari)

5.Zingatia ujenzi wa choo bora na matumizi sahihi choo

6.Kuacha tabia ya kunawa mikono katika chombo kimoja

7.Nawa mikono yako mara kwa mara kwa maji tiririka na sabuni


ZINGATIA NYAKATI HIZI KWA USAFI WA MIKONO

(Baada ya kutoka chooni, kabla ya kuandaa chakula, kabla na baada ya kula, baada ya kumsafisha mtoto alie jisaidia).


JALI AFYA YAKO, JIKINGE NA MAGONJWA YA KUHARISHA

read more
MTINDO BORA WA MAISHA NA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA
FAHAMU UGONJWA WA HOMA YA NYANI MPOX
HOMA YA INI

Kitaalam, ugonjwa huu wa ini   husababishwa na virusi vya Hepatitis B(HBV)ambayo vinathiri  mifumo wa utoaji wa sumu katika  mwilini wa binadamu. Inaaminika kwamba robo tatu ya watu ulimwenguni  wameathiriwa na vinyemelea vya  homa ya ini na wengine milioni 350 wameathirika moja kwa moja. 

 SABABU ZINAZOPELEKEA KUPATA HOMA YA INI

  • Ulevi wa kupindukia hasa kwa wale wanaotumia mapombe ya kienyeji ambayo hayana kiwango.
  • Sumu inapoingia mwilini ( chakula, chenye sumu).
  • Kuambukizwa kwa kufanya tendo la ndoa kwa kushikana na majimaji ya mwili wa mtu aliyeathirika ikiwa ni pamoja na damu, mate, machozi na mkojo.

DALILI ZA HOMA YA INI.

Ugonjwa ini huchukua muda mrefu  kuonekana na zikionekana mgonjwa anakuwa tayari amekwisha athirika sana.

  • Kuumwa na kichwa bila mpangilio.
  • Kusikia kichefu chefu
  • Kukosa hamu ya kula na kupungua uzito
  • Maumivu makali ya tumbo upande wa ini
  • Macho na ngozi kubadilika na kuwa rangi ya manjano ya njano
  • Choo kibwa na na kidogo kuwa  na rangi  ya manjano.
  • Kuvimba tumbo katika hatua za mwisho

Kwa maelezo zaidi tembelea katika Hospitali yetu ikiwa una dalili kadhaa.

read more