Barua Pepe | Facebook | Instagram | Twitter |

Rasilimali Watu

KUHUSU IDARA/KITENGO

  • Rasilimali watu katika Hospitali yetu ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara inaongozwa na watu wawili na ni mojawapo ya nyenzo muhimu katika kutoa huduma bora za afya. Serikali imefanya jitihada katika kuboresha rasilimali hii kwa njia mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuongeza idadi ya wataalamu, kuboresha ujuzi katika nyanja mbalimbali. 
  • Hii idara/kitengo kina lengo la kuziwezesha idara/vitengo vingine kutimiza majukumu yake, kutoa utaalamu na huduma mbalimbali zinazohusiana na usimamizi wa Rasilimaliwatu na Utawala kwenye Hospitali.


Majukumu ya idara/kitengo 

  • Kuratibu masuala ya Mahusiano na Ustawi wa Wafanyakazi ikiwa na pamoja na masuala ya Afya, Usalama, Michezo na Utamaduni
  • Kuratibu maandalizi, utekelezaji, usimamizi na tathimini ya Mkataba wa Huduma kwa Mteja hapa Hospitalini.
  • Kutoa huduma za Masijala, Ofisi na utunzaji na usimamizi wa kumbukumbu
  • Kutoa huduma za Kiitifaki hapa Hospitali
  • Kuratibu huduma za Ulinzi, Usafi na utunzaji Ofisi, majengo na maeneo/viwanja vya ofisi na huduma za Usafiri
  • Kutoa huduma za ujumla za uangalizi wa vifaa vya ofisi na majengo
  • Kuratibu utekelezaji wa jukumu la kuimarisha Nidhamu ikijumuisha utoaji wa elimu ya kuzuia Rushwa.
  • Kuratibu utekelezaji wa masuala mtambuka kama Jinsia, Ulemavu, HIV/AIDS hapa Hospitali.
  • Kushirikiana na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma – Tume/Sekretarieti ya Ajira na Wizara juu ya masuala yote yanayohusiana na Ajira na Uteuzi wa watumishi.
  • Kushauri juu ya ufanisi wa kitaasisi wa Hospitalini.
  • Kusimamia hatua/Mchakato wa kuwathibitisha na kuwapandisha vyeo/madaraja watumishi wa Hospitalini.
  • Kuwezesha mafunzo ya rasilimali watu na maendeleo (taaluma, weledi, kuboresha ujuzi) kwa ajili ya Hospitali
  • Kuwezesha programu za mafunzo elekezi kwa waajiriwa/watumishi wapya
  • Kusimamia Mpango wa Rasilimali watu kwa ajili ya kujua upatikanaji na mahitaji ya wataalamu kwenye Hospitali
  • Kusimamia mishahara na kushauri juu ya kusimamia mfumo/orodha ya malipo ya mshahara
  • Kusimamia utekelezaji wa mfumo wa wazi wa mapitio na upimaji wa utendaji wa kazi (OPRAS)
  • Kushughulikia na kuhusisha taarifa za watumishi kama Likizo za mwaka, likizo za uzazi na matibab, ruhusa za mafunzo/masomo na watumishi kuondoka kazini
  • Kuratibu upatikanaji wa mafao ya watumishi (malipo ya pensheni n.k) na madai mengineyo
  • Kushughulikia upatikanaji wa huduma zinazohusiana na watumishi kuondoka kwenye utumishi (kustaafu, kujiuzulu n.k)
  • Kuratibu kamati ndogo ya Ajira na Uteuzi ya Hospitali
  • Kusimamia masuala ya kinidhamu
  • Kuratibu na kushughulikia malalamiko na mashitaka
  • Kumshauri Mkurugenzi wa Hospitali juu ya masuala yanayohusu rasilimali watu
  • Kusimamia upatikanaji wa huduma za Habari, Elimu na Mawasiliano kwa ajili ya Hospitali
  • Kuratibu utekelezaji wa sera ya Menejimenti ya Utumishi wa Umma na sheria nyingine zinazohusiana na Utawala na Menejimenti ya Utumishi wa Umma.

Menejimenti ya Hospitali yetu inashiriki kikamilifu kwenye uandaaji wa makisio ya bajeti za mishahara ya watumishi kulingana na mwongozo wa Ikama iliyoidhinishwa na kuwasilisha kwa Katibu Mkuu kila mwaka wa fedha. Aidha, uongozi wa Hospitali unahahikisha unasimamia watumishi waliopo kwenye maeneo yao husika ili kuwezesha utoaji wa huduma bora kwa viwango vinavyokubalika. Usimamizi wa watumishi unatakiwa kuzingatia sheria, taratibu na kanuni za utumishi wa umma zilizoidhinishwa na mamlaka husika na hili litaenda sanjari na utoaji wa maslahi na haki mbalimbali za kiutumishi. Kwa kuzingatia hili, Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara inatoa motisha kwa watumishi kwa kuzingatia sheria, taratibu, kanuni na miongozo mbalimbali iliyopo. Aidha, Hospitali hii inandaa taarifa za mafao ya kustaafu kwa watumishi wake na kuwasilisha kwenye mamlaka husika kwa wakati na kwa kuzingatia taratibu za utumishi wa umma.