Barua Pepe | Facebook | Instagram | Twitter |

Ugavi na Manunuzi

KUHUSU KITENGO

  • Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara ina Afisa Mgavi mmoja ambae anazingatia Sheria, taratibu na kanuni za Manunuzi ya Umma. Katika utekelezaji wa sheria hii ya manunuzi, lazima suala la uwazi, uwajibikaji na uadilifu lizingatiwe katika michakato yote ya manunuzi itakayofanywa na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa.  Hospitali yetu inalazimika kuandaa mpango wa manunuzi unaotokana na mpango wa uendeshaji ulioidhinishwa wa kila mwaka (CHOP). Mpango huo hutawasilishwa kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya (Afisa Masuuli), ndani ya siku 30 baada ya bajeti ya mwaka husika kupitishwa na Bodi ya Hospitali.
  • Kitengo hiki kina lengo la kuleta ufanisi na kutoa huduma kwenye nyanja za manunuzi, utunzaji na usambazaji wa bidhaa na huduma mbalimbali zinazohitajika kwa ajili ya Hospitali. 


Majukumu ya Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi

  • Kushauri uongozi juu ya masuala yanayohusiana na manunuzi ya bidhaa na huduma na mchakato mzima wa kusimamia na kudhibiti mwenendo wa bidhaa na huduma katika Hospitali.
  • Kuhakikisha kwamba Hospitali inafuata/unatii taratibu za manunuzi kulingana na sheria ya Manunuzi ya Umma
  • Kuandaa na kufanikisha utekelezaji wa Mpango wa Mwaka wa Manunuzi kwa ajili ya Hospitali.
  • Kununua, kuhifadhi na kusimamia usambazaji, vifaa na huduma mbalimbali ili kukidhi mahitaji ya bidhaa na huduma hizo kwenye Hospitali.
  • Kuhakikisha kunakuwepo na utunzaji, uhifadhi sahihi na usambazaji wa mahitaji ya ofisi wa kutosheleza na kwa wakati
  • Kutunza na Kuboresha kumbukumbu ya vifaa na rasilimali za serikali/za Hospitali.
  • Kushughulikia uratibu wa kikao cha bodi ya manunuzi ya Hospitali kwa mujibu wa sheria ya manunuzi ya Umma ya mwaka 2011 na kanuni zake za mwaka 2013
  • Kuteketeza vifaa/vitu ambavyo havihitajiki