Barua Pepe | Facebook | Instagram | Twitter |

Uhusiano na Mawasiliano

KUHUSU KITENGO

 

Majukumu ya Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano

 • Kusimamia sera, mikakati na miongozo inayotolewa na Serikali Kuu juu ya uendeshaji wa kazi za habari na mahusiano
 • Kuandaa mpango, bajeti, mpango kazi, mpango mkakati wa kutekeleza kazi za habari na mahusiano katika Hospitali
 • Kutangaza na kuchapisha kazi na miradi inayofanyika katika Hospitali
 • Kutangaza maeneo ya uwekezaji ya Hospitali katika tovuti, radio, magazeti na majarida
 • Kuhakikisha tovuti ya Hospitali ina taarifa mpya kila wakati pamoja na Hospital Profile
 • Kuandaa na kutoa majarida kuhusu Afya
 • Kushiriki katika mijadala ya jamii kuhusu masuala ya Afya.
 • Kutumia TEHAMA katika kutoa elimu kwa jamii
 • Kusimamia press briefing za Hospitali
 • Kushauri Hospitalii juu ya uandaaji, uzalishaji na usambazaji wa nyaraka kwa wadau mbalimbali
 • Kushirikiana kwa karibu na afisa habari na uhusiano wa Mkoa na wa Wizara ili kubadilisha uzoefu na kujengeana uwezo.
 • Kutengeneza ,maktaba ya picha za mnato na video za hospitali.
 • Kuandaa na kushiriki maonyesho mbalimbali yanahusiana na Afya kwa kutengeneza vipeperushi na makala za maonyesho husika.
 • Kuhamasisha shughuli mbalimbali za Hospitali za kimkoa kwa kutumia vyombo vya habari