Huduma za Watoto
KUHUSU IDARA
- Idara hii inatumia wataalam waliobobea katika maswala ya matibabu ya watoto. Watoto bado wanakua, miili yao inabadilika wakati wote, miili yao ni midogo na wana hatari zaidi ya mabadiliko, wanaweza kuathiriwa na magonjwa haraka sana. Daktari wa watoto ni mtaalamu aliebobea maswala ya watoto. Kwa homa au joto kali au vipele kwa mtoto wako unahitaji kumuona daktari wa watoto, hali za kawaida zinaweza kutibiwa na daktari yeyote. Lakini unapaswa kutafuta msaada wa daktari wa watoto wakati mtoto wako anakuwa na hali ya kubadilika ghafla, au kuendelea na hali yoyote ambayo inazidi kuwa mbaya.