Barua Pepe | Facebook | Instagram | Twitter |

Uhasibu

KUHUSU KITENGO

Hospitali yetu ya Rufaa Mkoa wa Manyara ina jumla ya wahasibu watatu wanaoendesha shughuli mbalimbali za kimapato na malipo hapa hospitalini, katika kufanikisha hilo hospitali inatumia mifumo ya kielektronikia ya AfyaCare na GePG katika kukusanya mapato na menejementi inawajibika kudhibiti ukusanyaji wa mapato na matumizi.

Majukumu ya kitengo cha Fedha na Uhasibu yamegawanyika kwenye nyanja zifuatazo:

Usimamizi wa Mishahara

  1. Kuandaa na kuidhinisha malipo ya Mishahara
  2. kuandaa na kutunza orodha ya watumishi wanaolipwa mishahara
  3. Kuwezesha makato mbalimbali kutoka mishahara ya watumishi na kuyawasilisha mamlaka husika

Kuwezesha Malipo

  1. Kuandaa na kuingiza malipo kwenye mtandao wa malipo
  2. Kuchukua hundi za malipo kutoka Hazina ndogo
  3. Kupeleka fedha tasilimu na hundi benki
  4. Kutayarisha taarifa za mwezi za malipo
  5. Kuwalipa watumishi fedha taslimu au hundi na kuwalipa watoa huduma kwa hundi
  6. Kutunza daftari la hesabu

Hesabu za Mwisho wa Mwaka

  1. Kutayarisha Makadirio ya bajeti na kudhibiti matumizi
  2. Kuandaa taarifa ya matumizi ya robo mwaka, nusu mwaka na mwaka mzima kwa ajili ya kuiwasilisha kwa Mhasibu Mkuu wa Wizara
  3. Kuandaa taarifa ya hesabu za mwisho wa mwaka na kuziwasilisha kwa Mhasibu Mkuu wa Wizara 

Ukusanyaji Mapato

  1. Kukusanya Mapato
  2. Kusimamia mapato kwa mujibu wa sheria na miongozo

Ukaguzi wa Awali

  1. Kuhakiki nyaraka za malipo kama zimezingatia taratibu za malipo ikiwa ni pamoja na kuidhinishwa
  2. Kuhakikisha kama sheria, kanuni na miongozo na nyaraka za fedha kama zimezingatiwa
  3. Kuhakikisha malipo yatakayofanyika hayavuki bajeti ya kasma husika

Vyanzo vya mapato vitatokana na;

  • Ruzuku kutoka Serikali kuu
  • Papo kwa papo (User fees)
  • Bima za Afya (NHIF, CHF, na nyinginezo)
  • Fedha za Mfuko wa Dawa (Drug revolving Fund)
  •  Wadau wa maendeleo na wafadhili mbalimbali

Vyanzo vingine vinavyoibuliwa na hospitali yetu (harambee, kliniki tembezi za madaktari bingwa)