HOMA YA INI
Posted on: October 17th, 2019Kitaalam, ugonjwa huu wa ini husababishwa na virusi vya Hepatitis B(HBV)ambayo vinathiri mifumo wa utoaji wa sumu katika mwilini wa binadamu. Inaaminika kwamba robo tatu ya watu ulimwenguni wameathiriwa na vinyemelea vya homa ya ini na wengine milioni 350 wameathirika moja kwa moja.
SABABU ZINAZOPELEKEA KUPATA HOMA YA INI
- Ulevi wa kupindukia hasa kwa wale wanaotumia mapombe ya kienyeji ambayo hayana kiwango.
- Sumu inapoingia mwilini ( chakula, chenye sumu).
- Kuambukizwa kwa kufanya tendo la ndoa kwa kushikana na majimaji ya mwili wa mtu aliyeathirika ikiwa ni pamoja na damu, mate, machozi na mkojo.
-
DALILI ZA HOMA YA INI.
Ugonjwa ini huchukua muda mrefu kuonekana na zikionekana mgonjwa anakuwa tayari amekwisha athirika sana.
- Kuumwa na kichwa bila mpangilio.
- Kusikia kichefu chefu
- Kukosa hamu ya kula na kupungua uzito
- Maumivu makali ya tumbo upande wa ini
- Macho na ngozi kubadilika na kuwa rangi ya manjano ya njano
- Choo kibwa na na kidogo kuwa na rangi ya manjano.
- Kuvimba tumbo katika hatua za mwisho
Kwa maelezo zaidi tembelea katika Hospitali yetu ikiwa una dalili kadhaa.