ELIMU YA LISHE
Posted on: November 23rd, 2019Lishe bora maana yake ni kula chakula cha kutosha na chakula chenye virutubisho vyote muhimu. Lishe bora husaidia mwili kukua vyema, kuujenga mwili lakini pia huimarisha kinga ya mwili ili kuweza kupigana na magonjwa. Ili lishe iwe bora ni muhimu iwe na mchanganyiko wa vyakula mbalimbali kama vile protini, wanga, fati, mbogamboga, madini, matunda na maji kwa wingi .