ELIMU YA MAGONJWA YA TUMBO YANAYOSABABISHA KUHARISHA
Posted on: April 23rd, 2024Magonjwa haya ni kama vile homa ya tumbo (typhoid), kipindupindu, amoeba na minyoo. Haya ni magonjwa yanayosumbua jamii zetu kwa kiwango kikubwa. Yanasababishwa na kunywa au kula chakula chenye vimelea vya magonjwa hayo.
NJIA YA KUSAMBAA KWA MAGONJWA HAYA NI KAMA VILE;
1.Kula chakula au kunywa kinywaji kilicho na vimelea vya ugonjwa
Kunywa maji ambayo hayajachemshwa
Kula chakula kilichoandaliwa mazingira ambayo siyo safi
Kula matunda na mboga mboga ambazo hazijaoshwa vizuri
Kula chakula ambacho hakijafunikwa na kimepoa
2.Kutofuata kanuni na miongozo ya unawaji wa mikono
Kunawa mikono kwenye chombo kimoja
Kulisha mtoto bila kunawa mikono kwa sabuni na maji tiririka
Kutonawa mikono baada ya kutoka chooni
Kula chakula bila kunawa mikono kwa maji na sabuni
Kuandaa chakula bila kusafisha mikono
Mama kutonawa mikono baada ya kushika kinyesi cha mtoto
3.Kutofuata ujenzi wa choo bora na matumizi sahihi ya choo
4.Kuchafua vyanzo vya maji kwa kutirirsha maji ya choo kuelekeza kwenye mito na mifereji
5.Utupaji hovyo wa taka katika mazingira yetu kama vile majumbani,sokoni na minadani
NJIA YA KUJIKINGA NA MAGONJWA HAYA NI KAMA VILE;
1.Kusafisha mazingira yetu na kutoa taka zote ambazo ni hatari kwa afya zetu
2.Kuchemsha maji ya kunywa na kuhifadhi katika chombo kisafi chenye mfuniko imara
3.Kuandaa chakula katika mazingira safi na kukifunika kabla hakijatumika
4.Safisha vizuri kwa maji safi na tiririrka vyakula vinavoliwa vibichi kama vile matunda, mbogamboga na saladi (kachumbari)
5.Zingatia ujenzi wa choo bora na matumizi sahihi choo
6.Kuacha tabia ya kunawa mikono katika chombo kimoja
7.Nawa mikono yako mara kwa mara kwa maji tiririka na sabuni
ZINGATIA NYAKATI HIZI KWA USAFI WA MIKONO
(Baada ya kutoka chooni, kabla ya kuandaa chakula, kabla na baada ya kula, baada ya kumsafisha mtoto alie jisaidia).
JALI AFYA YAKO, JIKINGE NA MAGONJWA YA KUHARISHA