TEHAMA
KUHUSU KITENGO
Kitengo kina watumishi ambao ni Afisa TEHAMA. Toka kuanzishwa kwake hadi sasa kitengo hiki kimejitahidi kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa ili kuweza kufanikisha lengo namba 9 la Serikali ambalo ni kuimarisha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano. Jukumu kubwa la kitengo hiki ni Kusimamia masuala yote ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ya Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Manyara halikadhalika kusimamia mifumo yote ya Hospitali.
Majukumu ya Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
- Majukumu mengine ya msingi ya Kitengo yanahusu kusimamia kuratibu na ushauri wa matumizi ya teknolojia ya kompyuta.
- Kuhifadhi taarifa na Kumbukumbu za wadau na watumishi kwenye mifumo, pamoja na utekelezaji wa sera ya Serikali Mtandao (e-government policy) katika utumishi wa umma.
- Aidha, Ofisi hii ina jukumu la kupokea na kushughulikia malalamiko ya wadau yanayohusu Tehama.
- Kuhakikisha hospitali inatumia barua pepe za serikali (Government Mailing System) kwa ajili ya kutuma na kupokea taarifa za kiserikali.
- Kusimamia mawasiliano ya ndani ya hospitali (Internal Communication)
- Kusimamia Mifumo yote ya Hospitali, mifumo inayosimamiwa ni CTC2 Database, DHIS2, HRHIS, NHIF na bima nyingine, Afya-eHMIS, GePG, PEPMIS na NeST.
- Kusimamia matengenezo yote ya vifaa vya Tehama kwa kuhakikisha vifaa vyote vipo katika hali nzuri.