ELIMU YA USAFI
Posted on: November 23rd, 2019- Kama tunavyojua usafi wa mazingira na mwili ni njia ya kuendeleza afya kwa kuzuia mawasiliano ya binadamu na athari za taka. Usafi kama njia ya kuzuia maradhi inaweza kutumika kwa usahihi kabisa ili kuzuia maradhi na milipuko ya magonjwa mbalimbali hivyo ni muhimu kufanya usafi katika mazingira yanayokuzunguka lakini pia kunawa mikono kwa maji safi na sabuni baada ya kutoka chooni.
- Upungufu wa usafi wa mazingira ni sababu kuu ya maradhi duniani kote. Uboreshaji wa usafi wa mazingira una manufaa makubwa kwa afya ya wote katika kaya na katika jamii. Usafi wa mazingira unahusu pia udumishaji wa ratiba ya usafi, kwa njia ya huduma kama vile ukusanyaji wa taka na maji machafu.
