Barua Pepe | Facebook | Instagram | Twitter |

ZAIDI YA WANANCHI 500 WAFANYIWA UCHUNGUZI WA MACHO, 62 WAGUNDULIKA NA MTOTO WA JICHO

Posted on: December 18th, 2024

Katika Kliniki ya Upimaji na Uchunguzi wa Macho iliyofanyika kwa ushirikiano wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara, Shirika lisilo la Kiserikali, Kilimanjaro Center for Community Ophtalmology (KCCO) na Halmashauri ya Mji wa Babati katika Uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Wilayani Babati, Mkoa wa Manyara zaidi ya Wananchi 500 walijitokeza kufanya upimaji na uchunguzi wa macho kuanzia tarehe 16-17 Disemba 2024.

Kati ya wananchi hao zaidi ya 500, 62 waligundulika na mtoto wa jicho ambapo walipewa utaratibu wa kufika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara kwaajili ya matibabu zaidi siku ya jana tarehe 18 Disemba 2024.


Hata hivyo kwa waliogundulika na matatizo ambayo si ya upasuaji walipatiwa dawa na miwani.

Kliniki hii ya Upimaji na Uchunguzi wa macho itaendelea mwakani 2025 katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Manyara, alieleza Meneja Mradi KCCO Bi. Patricia Malley.