WIZARA YA AFYA YATOA MAFUNZO KWA WATUMISHI WA AFYA ILI KUBORESHA HUDUMA KWA MAMA NA MTOTO
Posted on: June 24th, 2025
Wizara ya Afya kupitia Kitengo chake cha Huduma za Mama na Mtoto imetoa mafunzo maalum kwa watumishi wa afya katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara, yenye lengo la kuwajengea uwezo wa kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili mama na mtoto.
Mafunzo hayo Yamefanyika kuanzia tarehe 21 hadi 25 Juni 2025 na yalihusisha watumishi kutoka wodi ya watoto wachanga, wodi ya wazazi, pamoja na kitengo cha upasuaji.
Kupitia mafunzo haya, watumishi walipata ujuzi na mbinu sahihi za utoaji huduma bora, ikiwemo utambuzi wa mapema wa hali hatarishi kwa mama na mtoto, hatua za haraka za kitabibu, pamoja na mbinu za kujenga mahusiano bora kati ya wahudumu wa afya na wagonjwa.