Barua Pepe | Facebook | Instagram | Twitter |

WIZARA YA AFYA - NIGERIA YATEMBELEA MANYARA RRH KUJIFUNZA HUDUMA ZA M-MAMA

Posted on: August 19th, 2025

Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara leo, tarehe 19 Agosti 2025, imepokea ugeni kutoka Wizara ya Afya ya Nigeria. Lengo la ziara hiyo lilikuwa kujifunza namna ya utekelezaji wa huduma za usafirishaji wa dharura wa mama mjamzito na mtoto mchanga (M-mama), pamoja na kutembelea  Kituo cha Kuratibu Usafirishaji wa Dharura za Mama na Mtoto (dispatcher center)

Wageni hao walifuatana na viongozi kutoka Wizara ya Afya Tanzania, Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), pamoja na wadau wa afya kutoka shirika la Pathfinder.

Kupitia ziara hiyo, wageni wamepata nafasi ya kujifunza kwa vitendo jinsi mfumo wa M-mama unavyosaidia kuokoa maisha ya mama na mtoto kwa kuhakikisha usafiri wa haraka na salama wakati wa dharura za uzazi.