Barua Pepe | Facebook | Instagram | Twitter |

WIKI YA KAMBI YA MADAKTARI BINGWA HOSPITALI YA RUFAA MKOA WA MANYARA

Posted on: March 26th, 2024

Katika muendelezo wa kuwasogezea huduma za matibabu karibu wananchi, Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara inaendesha kambi ya Madaktari Bingwa kutoka Hospitali za Mikoa na Kanda kwaajili ya kutoa huduma za matibabu kwa wananchi wa Mkoa wa Manyara na Wilaya jirani.

Kambi hii imeanza siku ya Jumatatu tarehe 25/03/2024 na jumla ya wananchi 285 walipata huduma ya matibabu.

Huduma ambazo zinapatikana katika kambi hii ni pamoja na magonjwa ya wanawake na uzazi, magonjwa ya ndani (Moyo, Sukari, Figo, na Presha), magonjwa ya upasuaji, magonjwa ya Pua, Sikio na Koo, Mifupa na Mgongo.

Jumla ya madaktari bingwa 14 kutoka Dodoma, Iringa, Arusha, Kilimanjaro na Tanga watatoa huduma katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara.

Hospitali inatarajia kupokea wananchi 1500 kadiri siku zinavyoenda hadi kufikia hitimisho tarehe 29/03/2024.