Waziri Ummy awapongeza Menejimenti ya Hospital ya rufaa ya Mkoa wa Manyara
Posted on: December 28th, 2023Leo 29. 12. 2023 Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu katika ziara yake Mkoa wa Manyara ametembelea Hospital ya rufaa Mkoa wa Manyara akiambatana na Mganga Mkuu wa Mkoa Dokta Damasi Kayera akimuwakilisha Katibu Tawala wa Mkoa, Mganga Mfawidhi Babu Meleyeki pamoja na Menejimenti ya Wataalamu kutoka Wiazara ya Afya.
Katika ziara hiyo Waziri wa Afya amepokea taarifa ya wagonjwa 5 ambao wamebaki wakipewa huduma sawa na hilo Waziri Ummy amechukua nafasi hiyo kuwa shukuru wafanyakazi wote na Menejimenti ya Hopsitali ya Mkoa kwakufuata uweledi na maadili na miiko ya kazi.
Pia amesisitiza juu ya Serikali kuhudumia majeruhi wote wa mapokomoko yaliyotokea Wilaya ya Hanang aidha amemshukuru Rais Samia Suluhu Hasani kwa uwekezaji mkubwa katiaka kuhakikisha Wananchi wa Wilaya ya Hanang wanaendelea kupata huduma zote muhimu.
Vilevile Waziri Ummy amepokea changamoto ya upungufu wa wodi ya upasuaji katika Hospital. Waziri ameipokea changamoto hiyo nakuitolea maelekezo ya kuipeleka katika Bajeti ya fedha ya mwaka 2024 -2025 sambamba na hayo Waziri Ummy ametembelea wodi ya wanawake, wodi ya watoto pamoja na wodi ya wanaume.
Pia, Dkt. Babu Meleyeki ambaye ni Kaimu Mganga Mfawidhi wa hospitali ya rufaa mkoa wa Manyara alimweleza Mh. Ummy kwamba kwa sasa majeruhi hao Watano waliolazwa wanaendelea kupatiwa matibabu.