Waziri Mkuu Kasim Majaliwa afurahishwa na huduma zinazotolewa hospitali ya Rufaa Mkoa wa Manyara
Posted on: December 4th, 2023Ziara ya Waziri Mkuu Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kasim Majaliwa akiambatana na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Sendiga, Naibu Waziri Wizara ya Afya Mhe. Godwin Mollel pamoja na Mganga Mkuu wa hospitali ya rufaa ya Mkoa Katherine T Magali wamefanya ziara katika hospitali ya Rufaa Mkoa wa Manyara.
Ambapo lengo la ziara hiyo ya Waziri Mkuu katika hospitali ni kutoa pole kwa majeruhi wa maporomoko ya udongo yaliyotokea Wilaya ya Hanang. Pia ziara hiyo imelenga kuangalia utendaji kazi wa Serikali kupitia idara ya maafa ambayo iko chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu.
Katika ziara hiyo Waziri Mkuu Kasim Majaliwa ametoa pongezi kwa madaktari na wauguzi katika hospitali ikiwa ni kuwapokea majeruhi na kuwapa huduma.
Aidha amefurahishwa na hali ya usafi pamoja na mazingira mazuri ya huduma za Afya zinazotolewa katika hospital ya rufaa ya Mkoa. Sambamba na hayo Waziri Mkuu ametembelea sehemu ya huduma kwa wateja.
Naibu Waziri wa Afya Mhe. Mollel katika ufafanuzi wake kuhusu hali ya utoaji huduma.Ameonyesha majeruhi wote wamepokelewa na kudumiwa pasipo garama zozote. Ikiwa niutekelezaji wa maelekezo ambayo yalitolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Maelekezo hayo ni Serikali kuhudumia wahanga wote wa maporoko hayo yaliyotokea Wilaya ya Hanang bure maelekezo hayo yamefanyiwa kazi na kutekelezwa katika hospital ya rufaa ya