Barua Pepe | Facebook | Instagram | Twitter |

WATUMISHI WA SEKTA YA AFYA TUENDELEE KUTUMIA BARUA PEPE ZA SERIKALI KWA MAWASILIANO

Posted on: June 1st, 2023
Msisitizo umetolewa na Watumishi wa Mamlaka ya Serikali Mtandao Bw. Ahmed Mtele na Bi. Queenter Mawinda wakati walipokuwa wakitoa elimu ya matumizi ya mifumo na barua pepe za serikali, kwa Watumishi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Manyara leo tarehe 1 Juni, 2023.
Akizungumza wakati wa mafunzo hayo Bi. Queenter Mawinda, mfumo wa barua pepe serikalini (GMS) ni mfumo unaowezesha Taasisi za Umma kuweza kuwasiliana na kubadilishana taarifa kati ya taasisi na taasisi kwa usalama, uhakika na kwa gharama nafuu. Mfumo huu unarahisisha mawasiliano kwa njia ya barua pepe kwa taasisi za serikali na kuongoza usalama wa taarifa zinazosafirishwa kupitia mfumo huu. ‘Watumishi wenzangu tunatakiwa kutuma nyaraka za serikali kwenye mfumo unaotambulika kwa mawasiliano ambao ni (GMS).’

Bi Queenter aliainisha majukumu ya Mamlaka ya Serikali Mtandao (EGA), EGA tunaimarisha na kuendeleza huduma za serikali mtandao kwa Taasisi za Umma, tunalitekeleza hili kwanza kwa kuongeza na kuboresha njia za utoaji wa huduma serikali mtandao, lakini vilevile tunatoa huduma za ushauri wa kimsaada wa kiufundi kwa taasisi za umma katika maeneo mbalimbali yanayohusiana na serikali mtandao, lakini pia tunawezesha upatikanaji wa miundo mbinu na mifumo salama na ya kuaminika kwa taasisi za umma yanayo husiana na serikali mtandao pia katika hili la kuimarisha tunaimarisha uratibu wa jitihada za usalama wa kimtandao katika taasisi za umma.
Naye Katibu wa Afya wa Hospitali Bi. Vailine Oswald alitilia mkazo kwa kumalizia, tujitahidi watumishi tutumie mifumo ya serikali mtandao.