Barua Pepe | Facebook | Instagram | Twitter |

WASANII WATOA POLE KWA MAJERUHI WA MAFURIKO YA HANANG, MANYARA RRH

Posted on: December 15th, 2023

Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao inayoongozwa na M/Kiti Steve Nyerere na Katibu Cherrie Khamis (Monalisa), wametembelea majeruhi wa mafuriko ya Hanang na wagonjwa waliolazwa katika wodi hospitalini hapa kwaajili ya kuwajulia hali na kuwapa zawadi mbalimbali, leo tarehe 15 Desemba, 2023.

Hata hivyo Kaimu Mganga Mfawidhi Dkt. Yesige Mutajwaa amewaeleza Wageni kwamba, majeruhi wengi wa ajali ya Hanang waliolazwa hospitalini hapa wameruhusiwa baada ya afya zao kuimarika na kwasasa wamebaki majeruhi wa tano (5) ambao bado wanaendelea na matibabu.