Barua Pepe | Facebook | Instagram | Twitter |

WANANCHI WA MBULU WAJITOKEZA KUFANYA UCHUNGUZI WA MACHO

Posted on: February 5th, 2025

Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara, kwa kushirikiana na Shirika la @kccoeyehealth , kwa udhamini wa Serikali ya Australia, imefanya uchunguzi wa macho kwa wananchi wa Kata ya Daudi, Wilaya ya Mbulu, lengo likiwa ni kupunguza changamoto ya matatizo ya macho inayowakabili wakazi wa maeneo hayo.

Uchunguzi huo umefanyika leo Februari 05, 2025 katika Kituo cha Afya cha Daudi, na umeweza kuwahudumia zaidi ya wananchi 480, Wengi wao wamepatiwa dawa na miwani ya macho.

Aidha Wananchi Zaidi ya 42 waligundulika kuwa na tatizo la mtoto wa jicho (Cataract), na watafanyiwa upasuaji wa kuondoa mtoto wa jicho kesho, Februari 6, 2025, katika Hospitali ya Wilaya ya Mbulu.

Uchunguzi huu ni sehemu ya mpango wa kuboresha huduma za afya za macho na kupunguza ulemavu unaosababishwa na matatizo hayo.