Barua Pepe | Facebook | Instagram | Twitter |

UZINDUZI WA KAMPENI YA UPANDAJI MITI ENEO LA ZIWA BABATI

Posted on: January 27th, 2023

Mkuu wa mkoa wa Manyara Mh. Charels Makongoro Nyerere akizindua kampeni ya upandaji miti 5,000 katika eneo linalozunguka ziwa Babati, inayoratibiwa na wadau wa mazingira ikiwemo Mati Superbrands Ltd, Miss Jangle na Mtandao wa Vikundi vya Wakulima na Wafugaji wa Mkoa wa Manyara (MVIWAMA). Uzinduzi huo uliambatana na zoezi la upandaji miti katika kitongoji cha Simbu, Kijiji cha Nakwa, kata ya Bagara mkoani Manyara leo 27. January, 2023. 

 “Swala la upandaji miti lisiishie tu kua jambo la kiserikali au wadau wachache bali kila mmoja wetu ajione anajukumu la kupanda miti, hivyo basi niwahimize tukalitekeleze hili katika maeneo yetu mbali mbali iwe maofisini au majumbani” Aliongea Mh. Makongoro

Katika Zoezi hilo Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Manyara ikiongozwa na Kaimu Mganga Mfawidhi Dkt Yesige Mutajwaa ilishiriki uzinduzi huo kama mdau wa mazingira kwa kupanda miti katika eneo linalozunguka ziwa Babati.