Barua Pepe | Facebook | Instagram | Twitter |

UZINDUZI WA BARAZA LA WAFANYAKAZI HOSPITALI YA RUFAA MKOA WA MANYARA

Posted on: March 22nd, 2024

Leo tarehe 22.03.2024 kimefanyika kikao cha uzinduzi wa Baraza la wafanyakazi katika Hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara. Kikao hicho kimehudhuliwa na Mganga Mfawidhi Dkt. Katherine Thomas Magali ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza, Makatibu wa Afya Hospitali ya Mkoa, Afisa Kazi Mfawidhi Bwn. Mwinyi Mkuu S. Mturuya, Bwn. Honest L. Temba ambaye ni Mwakilishi wa Katibu Mkuu TUGHE, Bwn. Tamson L. Mshighati ambaye ni Katibu wa TUGHE Mkoa wa Manyara.

Afisa Kazi Mfawidhi aliwapatia elimu wajumbe kuhusiana na sababu za kuunda Baraza hilo la wafanyakazi katika hospitali ikiwa ni pamoja na kuimarisha mahusiano mema kazini, kuimarisha dhana ya utawala bora pamoja na ushirikishwaji wa watumishi sambamba na kuimairisha ufanisi na tija katika sehemu ya kazi. Aliwapitisha pia wajumbe katika Sheria, Kanuni na taratibu za Utumishi wa Umma Na. 8 toleo la mwaka 2002 na Kanuni za mwaka 2003 GN. Na.168 Kanuni ya 107. Wajumbe walisisitizwa kuzingatia Sheria, Kanuni ,Miongozo na taratibu nyingine katika kuhakikisha Baraza linafanya kazi kwa ufanisi zaidi.

Katika kikao hicho cha Baraza la wafanya kazi umefanyika uteuzi wa majina ya Viongozi ambao ni Katibu wa Baraza na Katibu Msaidizi wa Baraza. Viongozi hawa walichaguliwa kwa kufuata demokrasia ya kupiga kura. Baada ya kupiga kura viongozi waliochaguliwa walikuwa ni Bwn. Freeman James Mutabilwa kama Katibu wa Baraza na Bi. Ketina Mallya kuwa Katibu Msaidizi wa Baraza la wafayakazi wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara.


Vilevile Baraza limefanya uchaguzi wa Muwakilishi wa Baraza kuu Wizara ya Afya ambapo Baraza liependekeza majina matano kwa ajili ya nafasi hiyo miongoni mwa majina hayo alipatikana mshindi ambaye amepata kura nyingi zaidi Bwn. Cosmas Charles Madembwe .


DHIMA YA UWEPO WA BARAZA LA WAFANYA KAZI

Nidhana nzima inayo husisha mahusiano mema katika sehemu ya kazi ikiwemo kuwapa motisha wafanyakazi sambamba na kusikilizwa na kutumia vipaji vya wafanyakazi ngazi ya chini hadi ya juu, pia utekelezaji wa misingi ya Utawala bora, ikiwemo kukuza ujuzi wa Wafanyakazi.


Aidha Baraza la wafanya kazi linajukumu la kuhakikisha kuna mahusiano mazuri kati ya Menejimenti na wafanya kazi wenyewe.