UVCCM WASHIRIKI KUFANYA USAFI NA KUWAJULIA HALI WANGONJWA
Posted on: October 11th, 2023Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Manyara wakiongozwa na Katibu Mkuu UVCCM Taifa Ndg. Fakii Lulandala na Viongozi wa UVCCM Mkoa, wameshiriki kufanya usafi na kuwajulia hali wagonjwa pamoja na kutoa zawadi kwa wagonjwa waliopo wodi ya Wazazi na Watoto, hospitalini hapa leo tarehe 11 Oktoba, 2023.
Ndg. Lulandala amepongeza uongozi wa hospitali kwa huduma bora wanazozitoa kwa wagonjwa wanaowahudumia. Pia amepongeza kwa usimamizi mzuri wa miradi iliyokamilika na inayoendelea.
Naye Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Manyara akiwakilishwa na Dkt. Suten Mwabulambo ameshukuru kwa ujio wa Katibu Mkuu Ndg. Lulandala na timu nzima ya UVCCM kwa kushiriki kufanya usafi na kutoa zawadi kwa wagonjwa waliopo hospitali na kuwakaribisha tena kwa kushiriki shughuli za kijamii.
Mganga Mfawidhi Dkt. Katherine Magali ameishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia fedha za ujenzi wa majengo (Radiolojia, Jengo la huduma za dharura na Jengo la ICU). Pia alimalizia kwa kushukuru serikali kuwapatia fedha za kununua vifaa tiba vinavyotumika kutolea huduma za afya hospitalini hapa.