USTAWI WA JAMII WAELIMISHA KUHUSU UTARATIBU WA KUWATEMBELEA WAGONJWA
Posted on: August 14th, 2025
Kitengo cha Ustawi wa Jamii cha Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara leo, Agosti 14, 2025 kupitia Kigoda cha Mteja, kimezungumza na ndugu waliokuja kuwaona wagonjwa hospitalini hapo.
Lengo lilikuwa kuwafahamisha kuhusu utaratibu mpya wa kuwatembelea wagonjwa wao ili kuongeza ufanisi, kuhakikisha usalama na faragha ya wagonjwa, pamoja na kurahisisha kazi za wahudumu wa afya.
Mbali na kutoa maelezo hayo, kitengo hicho pia kimesikiliza changamoto na kupokea maoni mbalimbali kutoka kwa ndugu hao kuhusiana na huduma zinazotolewa hospitalini, ili kusaidia kuboresha zaidi utoaji wa huduma.