SHULE YA SEKONDARI BAGARA YATOA POLE KWA WAGONJWA
Posted on: November 9th, 2022
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Manyara imetembelewa na wanafunzi wa kidato cha nne wa shule ya sekondari Bagara, ambao wanatarajia kufanya mitihani ya kitaifa tarehe 14/11/2022.
Zoezi hilo liliambatana na utoaji pole, maombezi na zawadi kwa wagonjwa kama sehemu ya sadaka zao.
Mwisho, walimu na wanafunzi walitoa neno la shukurani kwa uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara kwa mapokezi mazuri na kupata nafasi ya kuwatembelea wagonjwa.