Barua Pepe | Facebook | Instagram | Twitter |

SHULE 5 ZASHIRIKI KUFANYA USAFI WA MAZINGIRA KATIKA HOSPITALI YA MKOA WA MANYARA

Posted on: May 25th, 2024

Pichani ni Wanafunzi na Walimu wa Shule tano (5) za sekondari zilizopo H/Mji wa Babati mkoani Manyara pamoja na Afisa Afya Mazingira wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara Bi. Magdalena Mluta (kwa Niaba ya Uongozi wa Hospitali).

Kwa pamoja wanafunzi na walimu wa Shule za sekondari zikiwemo Kwaraa, Bagara, Nakwa, Angoni na Komoto wameungana kushiriki zoezi la usafi wa mazingira kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara ili kuweka mazingira safi ikiwa ni Jumamosi ya mwisho wa mwezi Mei 25, 2024 ambapo kila mwisho wa mwezi hufanyika usafi wa mazingira.

Katika zoezi hili la kufanya usafi wa mazingira hospitalini hapa, wanafunzi na walimu waliofika kushiriki zoezi hili waliambatana na wasimamizi wa project ya TELTA (Tanzania English language teachers association) ambao walielezea umuhimu wa project hii katika uhusiano na jamii.

“Project hii ni endelevu yenye lengo la kupromote Kiingereza shuleni pia kufundisha wanafunzi social skills kama vile kujitolea kwaajili ya jamii, kujenga uhusiano mzuri na jamii na kushiriki shughuli za kijamii” alieleza Afisa Uhusiano wa TELTA Bi. Happygod Macha.

“Hivyo tumeona ni vyema kusafisha mazingira ya hospitali, ikiwa kama kujitolea kwetu kuwaelimisha vijana wengine kuhusu kujitoa kwenye jamii na kugusa maisha ya wagonjwa kwa kuwawekea mazingira rafiki wawapo maeneo ya hospitali” aliongeza Bi. Happygod Macha.