PAROKIA YA ROHO MTAKATIFU YATEKELEZA MATENDO YA HURUMA KWA WAGONJWA
Posted on: February 9th, 2025
Waumini wa Kanisa la Katoliki Parokia ya Roho Mtakatifu Mjini Babati, wakiongozwa na Baba Paroko Thadeus Mosha Mshanga, wafanya matendo ya huruma kwa kutoa msaada kwa wagonjwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara, Lengo la tukio hili lilikuwa ni kuonyesha upendo na mshikamano kwa jamii, hasa kwa wagonjwa wanaohitaji msaada wa vitu vya kimsingi kama vile Maji,Sabuni na vinginevyo.
Akizungumza na waandishi wa habari, Februari 09, 2025, Baba Paroko Mosha amesema kuwa ni jukumu la Kanisa kueneza upendo na msaada kwa wale walio katika shida, hasa katika kipindi hiki cha changamoto za kiafya, Aliwataka waumini kuendelea kutoa msaada kwa watu wenye mahitaji na kuendeleza moyo wa kusaidiana katika jamii.
Msaada huo umeongeza faraja kwa wagonjwa na familia zao, huku wakishukuru kwa matendo ya huruma na upendo kutoka kwa waumini wa parokia hiyo.