Barua Pepe | Facebook | Instagram | Twitter |

"One Stop Center" kitakuwa tiba na suluhisho kwa Wanamanyara - RC Sendiga

Posted on: May 10th, 2024

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mh. Queen Cuthbert Sendiga ametoa wito kwa Wananchi wa Mkoa wa Manyara kufikisha matatizo ya vitendo vya ukatili kwenye Kituo Jumuishi cha Ukatili wa Kijinsia “One Stop Center” kilichopo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara ambacho ni maalumu kwa kusikiliza na kutafutia ufumbuzi matatizo hayo.

RC. Sendiga amesema hayo Mei 10, 2024 alipokutana na Afisa Maendeleo ya Jamii Bi. Anna Fisso, Wadau wa Afya na Vyombo vya Habari ofisini kwake.

RC. Sendiga amesema “uwepo wa kituo hiki ndio tiba na suluhisho kwa Wanamanyara katika kupata haki zao na kupambana na matukio ya vitendo vya kikatili”. 

Aidha RC. Sendiga amevipongeza Vyombo vya habari na Wanahabari kwa kutumia kalamu zao katika kuibua mambo na kusaidia katika mapambano ya kupinga vita dhidi ya ukatili.