Barua Pepe | Facebook | Instagram | Twitter |

MISS TANZANITE MANYARA ATEMBELEA HOSPITALI

Posted on: November 9th, 2023

Miss Tanzanite Manyara (2022-2023) Prisca Nangay, Mkurugenzi wa Natha’s Entertainment Bi. Aminatha Adolf Shamghe na Warembo wengine wakiongozana na Muuguzi Mfawidhi

Bw. Msafiri Sehaba wamefika leo hospitali ya Rufaa mkoa wa Manyara na kutembelea wodi ya wamama waliojifungua na wodi ya watoto kwaajili ya kuwajulia hali na kuwapatia zawadi mbalimbali.

Pia kwa pamoja wametumia fursa hii kuhimiza jamii kutembelea wagonjwa hospitalini ili kuwafariji.