Barua Pepe | Facebook | Instagram | Twitter |

Mhe. Queen Sendiga awajulia hali majeruhi wa ajali ya moto

Posted on: February 28th, 2024

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Sendiga akiambatana na kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa, Alitembelea Hopitalini hapa kwa lengo la kuwajulia hali majeruhi wa ajali ya moto.

Majeruhi hao walipata ajali ya moto mnamo tarehe 27 Februari, 2024 katika kiwanda cha ITRACOM kilichopo Wilayani Babati Mkoani wa Manyara. Mkuu wa Mkoa aliwapa pole majeruhi hao na kuwahakikishia kua watapokea huduma bora na zenye weledi kutoka  kwa madaktari na wauguzi Hospitalini hapa.

Vilevile Mkuu wa Mkoa ametoa pongezi kwa Mganga Mfawidhi Dkt. Katherine T. Magali kwa kuwapatia majeruhi hao huduma ya haraka ili kuweza kuendelea na hatua nyingine za matibabu.  

Wagonjwa hao wanaendelea kupokea matibabu na wako chini ya uangalizi maalumu wa kitabibu. Ziara hii ilihitimishwa kwa Mganga Mfawidhi kushukuru juu ya ujio huu wa Mkuu wa Mkoa ambao unaonesha uthamini wake kwa wananchi na kutambua mchango mkubwa wa hospital ya Rufaa ya Mkoa  katika utoaji wa huduma bora kwa wananchi Mkoani hapa.