MGANGA MKUU WA MKOA ASISITIZA HUDUMA BORA KWA WATEJA
Posted on: October 18th, 2024Mganga Mkuu wa Mkoa wa Manyara Dkt. Andrew Method ameshiriki kikao cha Watumishi cha Robo ya kwanza ya mwaka 2024/2025 kilichofanyika hapa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara siku ya jana Oktoba 18, 2024 na kuhudhuriwa na Viongozi na Watumishi wa hapa hospitali.
Dkt. Method ambaye alikuwa mgeni rasmi katika kikao hicho aliwasisitiza Watumishi kuendelea kutoa huduma bora kwa wateja wanaofika hapa hospitali ikiwemo huduma za afya.
Pia Dkt. Method aliongeza kwamba Watumishi wote kwa ujumla wanapaswa kushiriki katika kusimamia mapato ya ndani ya hospitali.
Kwa upande wa Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara Dkt. Katherine Magali alishukuru kwa ujio wa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Manyara na kuwataka watumishi kuendelea kusimamia kanuni, sheria, taratibu na miongozo ya utumishi ili kuendelea kutoa huduma stahiki kwa wateja.