Barua Pepe | Facebook | Instagram | Twitter |

MGANGA MFAWIDHI DKT. KATHERINE AFUNGUA MAFUNZO KWA WAHUDUMU WA AFYA

Posted on: September 9th, 2024

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara Dkt. Katherine Magali amefungua mafunzo ya tiba na upimaji kwa Wahudumu wa Afya kutoka hospitali na vituo vya afya vilivyopo mkoani Manyara, yanayofanyika katika ukumbi mkubwa hapa hospitalini.

Akimkaribisha wakati wa ufunguzi huo Prof. Pilly Chilo (Mkufunzi) amemweleza Mganga Mfawidhi Dkt. Katherine kwamba mafunzo haya yatakuwa na mazoezi ambapo wahudumu watapita hospitalini hapa kwa wagonjwa na kwenda kwenye jamii kufanya kile walichojifunza.


"Mafunzo haya yatajumuisha Management of Sore throat, Acute Rheumatic fever and Rheumatic heart disease in primary healthcare" Prof. Pilly alieleza.


Hata hivyo Dkt. Katherine Magali aliwasisitiza watahiniwa kwamba "mambo ambayo tutajifunza hapa tunapaswa kuyafanyia kazi na mwisho wa siku kuweza kuibua kile tulichotakiwa kuibua."

Mafunzo haya yanatarajiwa kufanyika kwa siku tano, kuanzia tarehe 9 - 13 Septemba, 2024 ambapo Wataalamu wa Magonjwa ya Moyo akiwemo Prof. Pilly Chillo (Cardiologist) ambaye aliongozana na wataalamu wengine kutoka Chuo Kikuu cha Muhimbili (MUHAS) wataendesha mafunzo haya kwa kushirikiana na wakufunzi wengine waliopo nchini South Africa kwa njia ya mtandao.