MEI 12 YAADHIMISHWA KWA KUWATEMBELEA WAGONJWA
Posted on: May 12th, 2025
Katika maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Duniani ambayo hufanyika tarehe 12 Mei kila mwaka, Wauguzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara wameadhimisha kwa kuwatembelea wagonjwa waliolazwa wodini na kuwapatia mahitaji mbalimbali.
Maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Duniani yamefanyika kitaifa Mkoani Iringa huku yakibeba kauli mbiu“Wauguzi nguvu ya mabadiliko duniani.”