Barua Pepe | Facebook | Instagram | Twitter |

MAKABIDHIANO YA HOSPITALI YA RUFAA MKOA WA MANYARA

Posted on: November 20th, 2019

Mnamo tarehe 21 Novemba, 2019, M. A. R Musa, Katibu Tawala Mkoa wa Manyara na Dkt. Katherine T. Magali Mganga Mfawidhi Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Manyara kwa niaba ya Dkt. Zainab Chaula, Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto waliidhinisha makabidhiano ya Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Manyara pamoja na rasilimali zake zote.

Katika shughuli hiyo ya makabidhiano, mhakiki mali, Bwana Hassan Majidu, Mganga Mkuu wa Mkoa, Dkt. Damas Kayera, Makatibu wa Hospitali ni miongoni mwa watu walioudhuria na kufanya zoezi liende kwa usahihi zaidi na kufanikisha kulikamilisha salama kabisa.

Kufuatia kuidhinishwa kwa makabidhiano hayo, Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Manyara na rasilimali zake zote zitasimamiwa na Mganga Mfawidhi Dkt. Katherine T. Magali kwa niaba ya Dkt. Zainab Chaula Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

Baada ya Katibu Tawala Mkoa wa Manyara, M. A R Musa kumkabidhi Hospitali Dkt. Katherine T. Magali, Dkt. Katherine T. Magali, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Manyara alisikika akisema "Pamoja na makibidhiano haya rasmi, tutaendelea kushirikiana kwa kila jambo kama ilivyokuwa awali"