Barua Pepe | Facebook | Instagram | Twitter |

MAGUGU NA DAREDA KATI WAPATIWA MAFUNZO YA MGUU KIFUNDO

Posted on: March 27th, 2025

Katika kuendelea kuwajengea uwezo watumishi wa afya katika kutoa huduma, Afisa Fiziotherapia Bi. Stella Mgema na Bi. Shamsa Kizera kutoka Idara ya Utengamao, Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara wameendesha mafunzo ya kuwahudumia watoto wanaozaliwa na mguu kifundo kwa Watumishi wa vituo vya Afya, Magugu na Dareda Kati vilivyopo Wilayani Babati, Mkoani Manyara.

Kwa upande wa watumishi waliopata mafunzo haya akiwemo Bw. Pasian Gurti wa Kituo cha Afya Dareda Kati ameeleza kwamba “kwa mafunzo tuliyopata yatasaidia kuwapatia huduma za awali watoto wenye mguu kifundo wanaopatikana katika maeneo yetu.

Hapo awali tulikuwa tunawapatia rufaa ya kwenda Hospitali ya Mkoa lakini kwa mafunzo tuliyopata tutaweza kugundua watoto wenye mguu kifundo na kutoa huduma za awali kabla ya kuwapa rufaa.”



Aidha mafunzo haya yaliyofanyika leo tarehe 27/03/2025 yenye lengo la kuwajengea uwezo watumishi wa afya yataendelea siku ya kesho tarehe 28/03/2025 katika Kituo cha Afya Gallapo, Wilayani Babati.