MAFUNZO YA LUGHA YA ALAMA KWA WATUMISHI WA AFYA
Posted on: August 17th, 2023Mapema leo watumishi wa Hospitalini hapa wamepewa mafunzo ya kuwasiliana na viziwi wakati wanapowahudumia.
Akizungumza Bw. Daud Donald ambaye ni Afisa Ustawi wa Jamii hospitalini hapa amesema “Kumekua na changamoto ya mawasiliano kwa wenye uziwi wanapofika kwenye huduma ya afya. Baadhi ya viziwi hushindwa kumuelezea mtoa huduma changamoto zake, hushindwa kuelewa matumizi ya dawa pale wanapopewa, kushindwa kuelewa mazingira ya hospitali kama vile sehemu ya dawa, wodi, vipimo n.k.
Kwa hivyo ni bora kushirikiana na viziwi kwa kuwa tayari katika kujifunza lugha ya alama, kujenga ushirikiano wapamoja na jamii ya viziwi na kutumia lugha ya alama ukiwa pamoja na viziwi.
Bw. Donald alitumia fursa hii kuwafundisha watumishi lugha za alama mbalimbali ambazo watatumia wakati wanawasiliana na viziwi kutoa huduma maeneo yao ya kazi.