Barua Pepe | Facebook | Instagram | Twitter |

WATUMISHI 34 WAHITIMU MAFUNZO YA 5S KAIZEN

Posted on: October 24th, 2025

Watumishi 34 wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara wakiwemo wafamasia, wauguzi, wataalam wa maabara, madaktari na kada nyinginezo, wamehitimu mafunzo ya uboreshaji wa maeneo ya kazi yanayojulikana kama 5S KAIZEN TQM.

Akizungumza wakati wa kuhitimisha mafunzo hayo jana Oktoba 24, Mganga Mfawidhi wa Hospitali Dkt. Yesige Mutajwaa amewasisitiza watumishi wote walioshiriki katika mafunzo kutumia kile walichokipata katika maeneo yao ya kazi kila siku. 

Dkt. Mutajwaa aliongeza kwamba eneo la usafi ni muhimu kuendelea kuimarika katika hospitali, hivyo kupitia mafunzo haya yakaimarishe eneo hilo.

Mafunzo ya 5S KAIZEN TQM yameendeshwa kwa siku 5 kuanzia tarehe 20 hadi 24 Oktoba, 2025 na hufundishwa kila mwaka ili kuwawezesha watumishi kuboresha maeneo yao ya kazi katika kutoa huduma kwa wateja.