MAFUNZO YA AWALI KWA WAAJIRIWA WAPYA YAANZA RASMI
Posted on: January 14th, 2025
Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara Dkt. Yesige Mutajwaa amefungua mafunzo ya awali kwa waajiriwa wapya Januari 13, 2025 yenye lengo la kuwasaidia waajiriwa kuelewa mazingira ya kazi, kuboresha ustadi wao na kuhakikisha kuwa wanakubaliana na maadili ya kazi ili kuchangia kwa ufanisi katika mafanikio ya ujumla ya hospitali ikiwa pamoja na kutoa huduma bora kwa wateja.
Mafunzo haya ya awali kwa waajiriwa wapya yalianza rasmi siku ya jana Jumatatu tarehe 13 Januari 2025 na yanatarajiwa kuhitimishwa tarehe 15 Januari 2025.