Barua Pepe | Facebook | Instagram | Twitter |

MADAKTARI WAIMARISHWA KATIKA USOMAJI WA KIPIMO CHA CT SCAN

Posted on: July 4th, 2023


Mafunzo ya usomaji na utumaji wa vipimo vya wagonjwa kwa ajili ya kufanyiwa kipimo cha CT Scan, yametolewa leo hospitalini hapa kwa madaktari na Dkt. Fides Canuty ambaye ni Mtaalamu wa Mionzi kutoka Hospitali ya Lutherani, Haydom. 

Dkt. Canuty amefafanua kuwa, utofauti uliopo kati ya X- Ray na CT Scan ni kwamba X-Ray hutoa picha ya moja kwa moja na hutoa picha moja (1) lakini CT Scan utoaji wake wa picha ni 3D na inatoa picha nyingi.

Mgonjwa aliyepata ajali hasa kwenye kichwa na mgonjwa mwenye uvimbe kichwani, shingoni, kifuani na tumboni wanatakiwa kupimwa kipimo cha CT Scan, Dkt. Canuty amesema.

Hata hivyo madaktari walifundishwa jinsi ya kusoma picha za CT Scan zilizopigwa katika sehemu tofauti za mwili wa binadamu.

Naye Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Manyara Dkt. Yesige Mutajwaa alihitimisha kwa kumpongeza Dkt. Canuty na madaktari waliohudhuria mafunzo.