Barua Pepe | Facebook | Instagram | Twitter |

MAAZIMISHO YA SIKU YA WAFAMASIA DUNIANI

Posted on: September 25th, 2022

Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara imeazimisha siku ya wafamasia duniani kwa kutoa elimu kwa jamii ya matumizi sahihi ya dawa.

Timu ya wafamasia kutoka hospitali ya mkoa,
wakiwemo:
1) Sungura Meshack (Mfamasia Kiongozi).
2) Renatus Kajogoo (Mfamasia).
3) Godwin Mutayoba (Mfamasia).
4) Elineema Mmary (Mfamasia).
5) Happiness Mosha (Mfamasia).
6) Bakari Rucha (Mfamasia).
7) Shukuru Robert (Mfamasia).

Walitoa elimu ya matumizi ya dawa kwenye shule tofauti tofauti zilizopo wilaya ya Babati zikiwemo shule ya sekondari Singe,shule ya sekondari Eloni na shule ya sekondari Hayatul Islamiya.

Wataalamu wa dawa walielimisha kwa kufafanua AINA 3 ZA MATUMIZI sahihi ya dawa ikiwemo :

Dawa sahihi: Wengi wamekuwa wakitumia dawa bila ya kufuata ushauri wa kitaalamu. Mgonjwa anapoumwa anakimbilia kununua dawa bila ya kupata ushauri. Nawashauri kufuata maelekezo sahihi ya wataalamu.

Dozi sahihi: Maswali ya kujiuliza ni je dozi unayotumia ni sahihi kwako ? je ni sahihi kwa umri wako ? je ni sahihi kwa uzito wako ?. Yote haya unapaswa kujiuliza kabla ya kuanza matumizi ya dozi ya dawa.

Matumizi sahihi ya dawa: Mgonjwa anaweza kuchukua muda mrefu bila kupona kutokana na matumizi yasiyo sahihi ya dawa. Ni heri ukaelewa tafsiri ya kile kilichoandikwa kwenye karatasi ya dawa kabla ya kuanza kutumia. Mfano mdogo: Dawa ikiandikwa 2x3 inafafanua kwamba, 2 meza asubuhi, 2 meza mchana na 2 meza jioni. Hii ina maana ya kwamba siku moja ina masaa 24 basi 24/3 (24gawanya3)

Pia Wataalamu waliongeza kwa kutaja faida na madhara ya matumizi ya dawa.
FAIDA ZA MATUMIZI SAHIHI YA DAWA: Kupona kwa wakati, kuimarisha kinga ya mwili na kupunguza vifo visivyo vya lazima.

MADHARA YA MATUMIZI YASIYO SAHIHI YA DAWA:
Kupoteza maisha, kuumwa kwa muda mrefu, kupata usugu wa dawa (tatizo la kupata usugu wa dawa linatokana na dawa kuzoa mwili na kupelekea ugonjwa kushindwa kupona), gharama kubwa (dawa ya kwanza inaposhindwa kutibu ugonjwa utahamishiwa kwenye kundi la juu la dawa).
na kuepuka kushindwa kwa matibabu (matumizi yasiyosahihi ya dawa yanapelekea kushindikana kwa matibabu).

Hata hivyo wataalamu wa dawa walimalizia kwa kutangaza huduma za madaktari bigwa waliopo hospitali ya mkoa wakiwemo: daktari bingwa wa sikio,pua na koo, daktari bingwa wa figo, madaktari bigwa wa magonjwa ya ndani (moyo,kisukari na presha), daktari bingwa wa macho, daktari bingwat wa uzazi na wanawake na daktari bingwa wa upasuaji.

Mwisho, shule zote kwa pamoja zilitoa shukrani za dhati kwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara kwa kutuma wataalamu wake kutoa elimu hiyo.