MAADHIMISHO YA WAUGUZI WAWAKUMBUKA WAMAMA WAJAWAZITO NA WATOTO WODINI
Posted on: May 17th, 2024Wauguzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara wamepita kwenye wodi za wazazi na watoto, kwa nia ya kuwapatia zawadi mbalimbali ikiwa ni katika kuadhimisha Siku ya Wauguzi Duniani inayofanyika kila tarehe 12 Mei kila mwaka.
Zoezi hili la ugawaji wa zawadi leo Mei 17, 2024 limeongozwa na Kaimu Muuguzi Msaidizi Bi. Josephine Mosha, ambapo pia alisema kwamba wameona ni vyema siku hii muhimu kuadhimisha kwa kuwakumbuka wagonjwa waliopo wodini kwa kuwapatia zawadi mbalimbali.
Katika wodi hizi walizogawa zawadi, Pia wagonjwa hawakuficha furaha zao na kuwashukuru wauguzi kwa namna ambavyo wamejitoa kuwa kumbuka wagonjwa waliolazwa wodini.
Ugawaji huu wa zawadi uliambatana na neno kutoka kwa Kaimu Mganga Mfawidhi Dkt. Yesige Mutajwaa ambapo aliwasihi wauguzi kuwekeza katika kujiendeleza kitaaluma ili waweze kuendana na huduma mpya na vifaa vya kisasa vya kutolea huduma kwa wagonjwa.