Barua Pepe | Facebook | Instagram | Twitter |

KILELE CHA MAADHIMISHO YA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA

Posted on: November 16th, 2024

Katika kuhitimisha Wiki ya Magonjwa yasiyoambukiza Kitaifa tarehe 16 Novemba 2024, Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara ilifanya upimaji wa magonjwa yasiyoambukiza na kuelimisha kuhusu magonjwa haya kwa Wakazi wa mkoa wa Manyara.

Watu mbalimbali walijitokeza kupatiwa huduma za upimaji wa kisukari, msukumo wa damu na uzito. Pia waliweza kupatiwa ushauri na saha pamoja na elimu ya kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza kutoka kwa Wataalam wa afya akiwemo Afisa Lishe na Mtaalam wa Afya ya akili.

Magonjwa yasiyoambukiza husababisha vifo vya watu milioni 41 kila mwaka duniani kote. Nusu ya wanaofariki ni wenye umri wa chini ya miaka sabini kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Duniani ‘WHO’, mwaka 2019.