Barua Pepe | Facebook | Instagram | Twitter |

Kikao cha Watumishi wote-Babati Manyara

Posted on: February 7th, 2020

Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Manyara imeadhimisha kikao cha watumishi wote tarehe 3, Februari, 2020 ambacho kiliongozwa na Bi. Mary Ntira Afisa Utumishi Mkuu kutoka Wizarani na Uongozi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Manyara ukiongozwa na Kaimu Mganga Mfawidhi Dkt. Elford M. Mukerebe.

Maadhimisho ya kikao hicho ilikuwa ilikuwa na lengo la kujadili na kutoa majibu mahsusi ya changamoto zinazowakabili watumishi wa hapa Hospitali na pia kuwapa njia mbadala za kufuatilia namna ya kutatua changamoto zinazowakabili.

Baadhi ya watumishi wakisikiliza kwa makini hoja zilizokuwa zikijadiliwa na uongozi toka Wizarani ukiongozwa na Bi.Mary Ntira Afisa Utumishi Mkuu.

Ni mengi sana yaliyojadiliwa, ikiwamo utaratibu wa watumishi katika kuomba mkopo, makato kutoka TUGHE na kuomba mbadala wa kila linaloonekana kuwa changamoto kwa watumishi katika utendaji kazi wao. Ziliweza kujadiliwa hoja nyingi kutoka kwa watumishi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Manyara na wengi wakilalamikia makato ya TUGHE bila ridhaa yao, mmoja wapo alinukuliwa akisema "Mimi swala la TUGHE bado sijalielewa kabisa, nilishajitoa uko na kujiunga kwingine nashangaa mwezi uliopita nikakatwa na huu tena nimekatwa sasa nataka kuuliza, Hela zangu nitazipataje??"

Wizara ilitoa majibu kwa kila hoja  na swali lililoulizwa toka kwa watumishi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Manyara, hivyo kuweza kufikia hitimisho la kikao hicho kwa kuweza kutoa shukrani kwa ushiriki wa watumishi kwenye kikao hicho na kuweza kufikisha hoja zao na kuweza kuzijadili ipasavyo.


Kutoka kushoto ni Bi. Sakina N. Kiponza Katibu wa Afya Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Manyara na Kulia ni Kaimu Mganga Mfawidhi Dkt. Elford M. Mukerebe pamoja na Afisa Utumishi katikati.

Baada ya kikao hicho, uongozi wa Wizara uliweza kukabidhi box moja la kinga kupitia kwa  Dkt. Elford M. Mukerebe na Katibu wa Afya Bi.Sakina N. Kiponza kama inavyoonekana kwenye picha hapo chini. Pia baada ya makabidhiano hayo wizara pamoja na uongozi ulipata picha ya pamoja kama kumbukumbu ya heshima kwa kuongoza shughuli nzima ya kikao na kumalizika vizuri kabisa.