KIKAO CHA WATUMISHI MACHI MOSI 2024
Posted on: February 29th, 2024Kikao cha watumishi kimefanyika leo na kuhudhuriwa na viongozi, watumishi na wageni kutoka chama cha wafanyakazi TUGHE wa mkoa wa Manyara
Kikao kiliambata na utoaji wa elimu kwa watumishi wanapohitaji kwenda kujiendeleza kimasomo na kupanda vyeo ambapo elimu hii ilitolewa na Afisa Utumishi Bi. Konjesta Marcel
Pia Muuguzi Mfawidhi Bw. Msafiri Sehaba kwa kushirikiana na kitengo cha ICU waliwasilisha taarifa ya hali ya utoaji huduma na maboresho ya kitengo cha ICU.
Wageni kutoka chama cha wafanyakazi TUGHE akiwemo Katibu wa chama na Katibu Msaidizi, walieleza dhana ya baraza la wafanyakazi kwa watumishi na kueleza kazi mbalimbali zinazofanywa na chama cha wafanyakazi.
Kikao hiki kilihitimishwa na Mganga Mfawidhi Dkt. Katherine Magali akiwasisitiza watumishi kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi wanaofika hospitalini hapa.