KATIBU TAWALA MANYARA NA MGANGA MKUU WA MKOA WAKAGUA HALI YA UTOAJI HUDUMA ZA MATIBABU
Posted on: December 29th, 2023Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara Bi. Maryam Ahmed Muhaji akiwa na Mganga Mkuu wa mkoa Dkt. Damas Kayera wamefika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Manyara kuangalia maendeleo ya afya za majeruhi wa Hanang’ pamoja na kukagua hali ya utoaji huduma kwa wagonjwa waliolazwa wodini.