IDARA YA MACHO IMEFANYA UCHUNGUZI KWA WATU WENYE MAHITAJI MAALUMU, BABATI
Posted on: May 15th, 2024Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara kwa kushirikiana na KCCO kwa msaada wa Watu wa Australia, kupitia Idara ya Macho wametoa elimu, uchunguzi kwa watu wenye mahitaji maalumu waishio Wilaya ya Babati, Mkoani Manyara leo Mei 15, 2024.
Huduma hii imejumuisha Viziwi, Wasioweza kuongea, Walemavu wa Viungo na Wangozi, Wazee, Wasioona ambapo Wataalamu kutoka KCCO, Hospitali ya Taifa Muhimbili, Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara na Watumishi wa Idara ya Maendeleo ya Jamii kutoka Halmashauri ya Mji wa Babati wameshiriki kutoa huduma kwenye eneo la Shule ya Kwaang’w, Babati.
“Zaidi ya watu 80 wenye mahitaji maalumu waliofanyiwa uchunguzi kati yao wamepatiwa miwani, dawa na 10 wameshauriwa kufika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara siku ya Alhamisi tarehe 16 Mei 2024 kwaajili ya matibabu zaidi ikiwemo upasuaji kwa wale wenye mtoto jicho” Alisema Meneja Mradi KCCO Bi. Patricia N. Malley.