Barua Pepe | Facebook | Instagram | Twitter |

IDARA YA DHARURA (EMERGENCY DEPARTMENT) YATOA MAFUNZO KWA WATUMISHI

Posted on: January 12th, 2023


Katika muendelezo wa utoaji ripoti za siku (Morning Reports) Idara ya Dharura iliendesha mafunzo mafupi juu ya Huduma za Dharura kuhusu ufufuaji wa mishipa ya moyo kwa kitaalamu inaitwa “Cardiopulmonary Resuscitation (CPR)”. Akiendesha mafunzo hayo, Dkt. Ezekiel Morris Lukenza alieleza maana ya CPR, muda gani wa kufanya CPR, umuhimu wake na namna ya utoaji. 

Akisisitiza juu ya umuhimu wa kila mtumishi kufahamu kuhusu huduma hii, Daktari alisema; “CPR ni kifupisho cha neno “Cardiopulmonary resuscitation” ikiwa na maana ya kufufua moyo na mapafu viweze kufanya kazi. Ni kitendo cha kubana kifua ili kuweza kurejesha mapigo ya moyo kwa mtu ambaye amepatwa na mshituko wa moyo na hii ufanyika pale ambapo tatizo limetokea papo hapo”.

“CPR inakazi mbalimbali na inawezesha kutoa msaada wa hali ya juu kuliko inavyofikiriwa. CPR inafanya kazi zaidi ya kuwezesha moyo kusukuma damu. CPR ni huduma ya kwanza inayowezesha kupelekwa kwa hewa safi ya oxygen kwenye ubongo na viungo vingine muhimu hadi mgonjwa atakapopata matibabu rasimi. CPR inampa mtu nafasi maradufu ya kumuokoa mara apatapo shambulio la mshtuko wa moyo. CPR inaokoa maisha ndio maana ni muhimu kila mmoja kujifunza mbinu hii”, alisisitiza Dkt.Ezekiel Morris Lukenza.

Mwisho kabisa alinukuu na kusema “kuchukua maamuzi sahihi haraka na kwa kujiamini kunaweza leta tofauti kubwa kati ya uhai na kifo kwa mtu anaekabiliwa na mshtuko wa moyo”.

#hudumaboraniwajibuwetu