Barua Pepe | Facebook | Instagram | Twitter |

HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA MANYARA YAADHIMISHA SIKU YA MTOTO NJITI DUNIANI

Posted on: November 18th, 2024

Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara, Idara ya Watoto, Kitengo cha Watoto Wachanga wamefanya hafla fupi siku ya jana tarehe 18/11/2024, kuadhimisha Siku ya Mtoto Njiti Duniani ambayo hufanyika Novemba 17 kila mwaka.

Hafla hii ili wakutanisha wamama ambao wamejifungua watoto kabla ya wakati (watoto njiti) na watoto ambao walizaliwa kabla ya wakati na sasa wanaendelea na maisha yao, akiwemo mtoto Samia Wilbroad miaka (6) (mwenye gauni la pichi pichani).

Inaelezwa kwamba sababu mbalimbali kama hatari za afya ya uzazi, kama vile mimba za utotoni, maambukizi, lishe duni, na hali ya kutokwa na damu wakati wa ujauzito, matumizi ya Pombe au dawa za kulevya ni sababu zinazohusishwa na kuchangia mama mjamzito kujifungua mtoto njiti.