HOSPITALI YA MKOA WA MANYARA YASHIRIKI TAMASHA LA JOGGING
Posted on: September 1st, 2024
1 Septemba, 2024
Watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara wameungana mapema leo Septemba 1, 2024 na Taasisi mbalimbali pamoja na wakazi wa Mji wa Babati kushiriki Jogging ya km 4, iliyoanzia Uwanja wa Tanzanite Kwaraa kuzunguka mjini na kuishia Uwanjani hapo kwa mazoezi.
Tamasha hili lililobeba jina la Manyara Daftari Day lilikuwa na lengo la uhamasihaji wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika tarehe 27 Novemba, 2024. Ambapo wananchi wa mkoani hapa walisisitizwa kuboresha taarifa zao katika daftari la kudumu la mpiga kura na hamasa zaidi kujitokeza kwa wingi kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Hata hivyo Viongozi mbalimbali walishiriki Tamasha hili akiwemo Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Daniel Sillo (Mb), Paulina Gekul (Mbunge Babat Mjini) na Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa, Viongozi mbalimbali wa taasisi za umma na binafsi pamoja.
Pamoja na tamasha hili la Jogging, wakazi mbalimbali wa Mji wa Babati walijitokeza katika uchangiaji wa damu kwa hiari na upimaji wa vipimo vya awali uwanjani hapo.
Tamasha hili la Jogging liliongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mh. Queen Sendiga ambapo lilibeba kauli mbiu “Imarisha Afya Yako, Jiandikishe na Kuchagua Viongozi wa Serikali za Mitaa kwa Ujenzi wa Jamii Endelevu.”