Barua Pepe | Facebook | Instagram | Twitter |

HOSPITALI YA MKOA IMESHIRIKI MAAZIMISHO YA SIKU YA WAFANYAKAZI MKOANI MANYARA

Posted on: April 29th, 2024

Maazimisho ya Siku ya Wafanyakazi, Mei Mosi yamefanyika leo tarehe 29 Aprili 2024 mkoani Manyara katika Uwanja wa Tanzanite Kwaraa ambapo Wafanyakazi wa Taasisi na Mashirika mbalimbali wameshiriki siku hii. 

Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Manyara imeshiriki kwenye maazimisho haya kwa kutoa elimu na huduma mbalimbali zikiwemo vipimo vya awali, elimu ya lishe, uchunguzi wa macho na elimu ya kifua kikuu.

Mkuu wa Wilaya ya Babati Mh. Lazaro Twange akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Manyara alikuwa mgeni rasmi kwenye maazimisho haya ambapo alipata wasaa wa kutembelea banda letu na kujionea huduma mbalimbali zinazoendelea kutoka kwa wataalam wetu wa idara na vitengo mbalimbali vya hospitalini hapa.

Kwa upande mwingine mgeni rasmi Mh. Mkuu wa Wilaya ya Babati akiwa na Mkurugenzi wa Mji, Katibu Tawala Wilaya ya Babati, Viongozi wa Wilaya za Mkoa wa Manyara na Viongozi wa vyama vya wafanyakazi mkoa waliwatunuku wafanyakazi bora vyeti, ambapo kwa upande wa Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Manyara Watumishi wawili (2) wa idara ya macho na idara ya mama na mtoto walitunukiwa vyeti vya wafanyakazi bora.